Ina maana gani kwamba mshahara wa dhambi ni mauti?

Warumi 6:23 inasema, "Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti; bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu." Katika msingi wake, dhambi ni uasi dhidi ya Mungu. Dhambi zetu hututenganisha na Mungu, Muumba na mwenye uzima. Yesu alisema, "Mimi ndimi njia na kweli na uzima" (Yohana 14: 6). Mungu anajulikana kama "MIMI NDIMI" mkuu. Uzima uu katika Mungu. Kwa hivyo, tunapofanya dhambi na kujitenganisha na Mungu, tunatengana na uzima wa kweli. Kwa hivyo, bila shaka, tunakumbana na mauti. Hoja tatu za ufafanuzi zinahitajika: Kwanza, dhambi hasa haisababishi kifo cha kimwili mara moja. Warumi 6 haituambii kwamba tunapofanya dhambi tutakufa kimwili. Badala yake, inarejelea kifo cha kiroho. Pili, wakati tunapookoka katika Kristo, tunaokolewa kutokana na hatima ya kifo cha kiroho na kuletwa katika hatima ya uzima wa kiroho. Paulo aliwaambia Warumi, "Zawadi ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu" (Warumi 6:23). Tatu, hata dhambi za waumini bila shaka zitasababisha aina ya "kifo" cha kiroho. Ingawa tumeokolewa kutokana na adhabu ya mwisho ya dhambi (kutengwa kwa milele na Mungu), hatuokolewa kutokana na matokeo ya asili ya uhusiano uliovunjika na Baba . Tunapofanya dhambi, tunapata dalili za kifo cha kiroho. Tunaweza kujihisi kuwa na hatia, kuwa wapungufu, kuchanganyikiwa, au kutokuwa na uhusiano na Mungu. Sisi hufanya kama waadilifu badala ya kuwa wenye haki. Dhambi zetu, hata kama waumini, huumiza moyo wa Mungu na uhuzunisha Roho Wake (Waefeso 4:30). Ingawa dhambi zetu haziachi uhusiano wetu na Yeye, huweka kizuizi kati yetu. Fikiria mtoto na mzazi. Wakati mtoto anapoasi, uhusiano na mzazi wake unafadhaika. Mzazi bado anampenda mtoto na bado ana nia bora kwa mtoto moyoni. Mtoto kamwe aachi kuwa bila mzazi. Hata hivyo, mtoto anaweza kupata matokeo fulani: kutoaminiwa, nidhamu, hisia ya hatia, na kadhalika. Bila shaka hatimaye uhusiano hurejeshwa ila kawaida pigo huja kwanza. Hivyo ni pamoja nasi na Mungu. Tunapoasi dhidi ya utawala wa Mungu katika maisha yetu, tunaasi dhidi ya Uzima, na hivyo tunakumbana na mauti (kuvunjika kunaosababisha maumivu). Tunapomrudia Mungu, tunarudishwa tena kwenye ushirika wa kiroho na Mungu, hisia za lengo, haki, uhuru, nk. Baba mwenye furaha katika mfano wa Mwana mpotevu alisema vizuri zaidi: "Huyu mtoto wangu alikuwa amekufa na yu hai tena "(Luka 15:24).

SIFA PEKEE ZA YESU KRISTO

 

Je umewahi kukutana na mtu ambaye ni nguvu ya kusikilizwa mahali pote aendapo? Baadhi ya sifa za mafumbo, zisizoelezeka kirahisi zimemtenga mbali na watu wengine wote. Kwa hakika, hivyo ndivyo ilivyokuwa miaka elfu mbili iliyopita kwa Yesu Kristo, lakini hiyo haikuwa tu tabia ya Yesu pekee iliyowavuta hao waliomsikia. Kwa hao walioshuhudia maneno na maisha yake wanatuambia jambo fulani kuhusu Yesu wa Nazareti kuwa alikuwa tofauti na watu wengine wote.

 

Sifa pekee za Yesu zilikuwa ni yeye mwenyewe. Hakuandika kitabu, hakuamrisha jeshi, hakushikilia ofisi ya kisiasa, wala hakumiliki mali. Hasa, alisafiri karibu maili mia moja za kijiji chake, akiwavuta makundi ya watu walioshangazwa kwenye maneno makali na matendo yake ya kushangaza.

 

Na pia ukuu wa Yesu ulikuwa wazi kwa hao waliomuona na kumsikiliza. Na wakati watu wengine maarufu hatimaye husahaulika kwenye vitabu vya historia, Yesu bado ni kitovu cha maelfu ya vitabu na majadiliano yasiyo na kifani kwenye vyombo vya habari. Na mengi ya majadiliano hayo yanazungukia kuhusu madai ambayo Yesu aliyafanya – madai ya msingi ambayo yaliwashangaza wote, wafuasi wake na maadui zake.

 

Hasa ni madai ya kipekee ya Yesu yaliyomsababishia aonekane kama tishio kwa Mamlaka za Kirumi na Tawala za Kiyahudi. Japokuwa alikuwa mgeni asiye na sifa wala nguvu za kisiasa, lakini ndani ya miaka mitatu, Yesu amebadilisha dunia kwa karne 20 zingine zijazo. Viongozi wengine wa kimaadili na kidini wameacha mfano – lakini si kama huo wa mtoto huyo wa Seremala wa kawaida kutoka Nazareti.

 

Ni kitu gani kuhusu Yesu Kristo ambacho kimeleta mabadiliko? Alikuwa ni mtu mkuu tu, au kuna kitu cha zaidi?

 

Maswali haya yaelekea kwenye kiini kwamba Yesu alikuwa ni nani hasa. Wengine wanaamini alikuwa tu ni mwalimu wa maadili makuu; wengine wanaamini alikuwa ni kiongozi tu wa dini kubwa duniani. Lakini wengine wanaamini zaidi ya hayo. Wakristu wanaamini kuwa Mungu kwa hakika alitujia duniani katika umbo la ubinadamu. Na wanaamini kwamba ushahidi unathibitisha hilo.

 

Mwalimu wa Ajabu

 

Hata hao toka katika dini zingine wanakiri kwamba Yesu alikuwa Mwalimu wa Maadili Mkuu. Kiongozi wa wahindi, Mahatma Gandhi, aliongelea mno maisha ya Yesu na maneno yake makuu ya busara.[1] Vile vile msomi wa Kiyahudi Joseph Klausner aliandika, “Inakubalika pote kwamba Kristo alifundisha maadili safi na makuu mazuri sana… ambayo yanapita mafundisho na maneno ya watu wa busara wa kale, wote waliowahi kutokea.”[2]

 

Mafundisho ya Yesu mlimani, yameitwa ni mafundisho bora ya binadamu, yaliyowahi kutamkwa na binadamu. Kwa kweli, mengi ya tujuayo leo kama “haki sawa” kwa kweli ni matokeo ya mafundisho ya Yesu. Mwanahistoria Will Durant, si-Mkristu, alisema kwamba Yesu aliishi na alipambana vilivyo bila kukoma kwa ajili ya ‘haki sawa’ katika nyakati za sasa angepelekwa Siberia. Aliwahi kusema yeye  ambaye ni mkuu miongoni mwenu , na  awe mtumishi wenu” hii ni kinyume na maono ya kisiasa ya ufahamu wote.[3]

 

Wengi kama Ghandi, wamejaribu kutofautisha mafundisho ya Yesu ya maadili kutoka katika madai yake kuhusu yeye mwenyewe, wakiamini alikuwa ni mtu tu mkuu ambaye alifundisha maadili lukuki – mengi. Hii ilikuwa ni njia ya mmoja wa Baba Waasisi, Rais Thomas Jefferson, ambaye alikariri na kunakili Agano Jipya, akiondoa sehemu zilizomzungumzia Uungu wa Yesu, akiacha vifungu vilivyojali mafundisho ya kiimadili ya Yesu.[4] Jefferson aliendelea na kukopi kwake na kunakili Agano jipya akimheshimu Yesu kama labda ni mwalimu mkuu kuliko wote wa maadili wa nyakati zote.

 

Kwa hakika, maneno ya kukumbuka ya Jefferson katika Tangazo la Uhuru yalijengwa ndani ya misingi ya mafundisho ya Yesu kwamba kila mtu ni wa umuhimu mkubwa na sawa kwa Mungu, bila kujali jinsi, taifa, rangi wala nafasi yake katika jamii.  Andiko maarufu laweka wazi, “Twashikilia kweli hizi kuwa ushahidi kwamba watu wote wameumbwa sawa, kwamba wamebarikiwa na Muumbaji kwa haki fulani sawa  zisizohamishika na zisizotwalika/twaliwa na mtu mwingine…”

 

Lakini kitu kimoja Jefferson hakukijibu: Ikiwa Yesu si kweli alidai kuwa Mungu, asingekuwa mwalimu mzuri wa maadili. Lakini ni kweli Yesu alidai Uungu? Kabla hatujaangalia kitu gani Yesu alidai, twahitaji kuchunguza uwezekano kwamba alikuwa tu kiongozi mkuu wa dini?

 

 

 

Kiongozi wetu mkuu wa dini?

 

Cha kushangaza, Yesu kamwe hakudai kuwa yeye ni kiongozi wa kidini. Hakuwahi kamwe kujiingiza au kulazimisha agenda za tamaa, na muda wote alihubiri nje ya idara za kidini.

 

Mtu anapomlinganisha Yesu na viongozi wengine wa kidini, tofauti kubwa yajitokeza. Ravi Zacharia, ambaye alikulia katika utamaduni wa ki-Hindu, amejifunza dini za duniani na amegundua tofauti kubwa kati ya Yesu Kristo na waasisi wa dini zingine.

 

”Katika yote haya, kunajitokeza, ufundishaji, mwenendo wa maisha. Na Si Zoroaster unayemgeukia; ni Zoroaster ambaye unamsikiliza. Si Buddha anayekukumboa; ni ukweli bora unaokuelekeza. Si Mohammad anayekubadilisha, ni uzuri wa Koran unaokuvutia. Tofauti na hayo, Yesu hakufundisha tu au kueleza ujumbe wake. Alifanana na ujumbe wake.”[5]

 

Ukweli wa Zakariya ‘kumweka unatokana na idadi ya mara katika Injili kuwa Yesu’ mafundisho ujumbe mara tu “Njoni kwangu” au “Nifuate” au “Mt’iini yangu.” Pia, Yesu aliweka wazi kwamba kazi yake ya msingi ilikuwa kusamehe dhambi, jambo ambalo Mungu pekee anaweza kufanya Katika dini kubwa za duniani.

 

Huston Smith aligundua, “Watu wawili tu ambao wamewastajaabisha wafuasi wao sana kiasi kwamba swali walilozingatia halikuwa ‘Ni nani Yeye?’ bali ni nini Yeye?’ Watu hao walikuwa ni Yesu na Buddha. Buddha alisema waziwazi kwamba alikuwa ni mtu tu, sio Mungu – kama vile aliwahi au alishaona majaribio ya kumwabudu yeye [Yesu]. Yesu kwa upande mwingine, alidai kuwa Mungu mtakatifu.[6]

 

Na hilo linatuongoza sisi kwenye swali la nini Yesu alifanya kudai mwenyewe; je, Yesu alidai kweli kuwa Mungu Mtakatifu

 

Yesu aliwahi kudai kuwa Mungu?

 

 “Marafiki na maadui wa Yesu waligawanyika tena na tena na kile alichosema na alichofanya [Yesu]. Alikuwa alitembea barabarani, dhahiri kama mtu yeyote, kisha akageuka na kusema kitu fulani mfano ‘Kabla ya Abraham kuwako, nipo.’ Au iIkiwa umeniona, basi umemuona baba. Kisha kwa utulivu baada ya kulaumiwa kukufuru, alisema, ‘Mwana wa Adamu ana mamlaka duniani kusamehe dhambi’ Kwa wafu, alisema ‘Njoo mbele’, au, ‘Inuka’ na walitii. Kwa tufani baharini aliweza kusema ‘Tulia’ na kwa kipande cha mkate, alisema ‘Kuwa vipande elfu moja’ na vilifanyika mara moja.”[7]

 

Lakini ni kitu gani Yesu alimaanisha kwa hayo maneno? Je, inawezekana Yesu alikuwa mtume tu kama Musa au Eliya, au Daniel? Hata usomaji wa juu juu wa Injili unadhihirisha kwamba Yesu alidai kuwa mtu fulani zaidi ya nabii. Na hakuna mtume mwingine aliyefanya hayo madai kujihusu, kwa kweli, hakuna mtume mwingine yeyote aliwahi kujiweka katika nafasi ya Mungu.

 

Baadhi ya watu wanadai hakuwahi waziwazi kusema “Mimi ni Mungu”. Ni kweli kwamba hakuwahi kunena maneno hayo? “Mimi ni Mungu”. Vilevile, Yesu hakuwahi waziwazi kusema “Mimi ni binadamu” au “Mimi ni nabii” Na Yesu alikuwa binadamu bila shaka, na wafuasi wake walimchukulia kama nabii kama Musa na Eliya. Kwa hiyo hatuwezi kuamua kwamba Yesu kuwa mtakatifu ni kwa sababu hakusema maneno hayo, kama ambavyo hatuwezi kusema hakuwa nabii.

 

Kwa kweli, kauli za Yesu kujihusu zinapinga na wazo kwamba alikuwa tu mtu mkubwa au nabii. Katika zaidi ya mara moja, Yesu alijiita Mwana wa Mungu. Wakati alipoulizwa kwamba alifikiria imezidishwa kwa Yesu kuwa Mwana wa Mungu, mwimbaji kiongozi wa U2 Bono, alijibu:

 

‘Hapana, haijazidishwa kwangu. Angalia mwitikio wa kawaida kwa simulizi ya Kristo siku zote huwa hivi. Alikuwa nabii mkubwa, dhahiri alikuwa mtu wa kuvutia, alikuwa na mengi ya kusema miongoni mwa mitume wengine wengi, kama Eliya, Muhammad, Buddha, or Confucius. Lakini kwa kwa kweli Kristo hakuruhusu jambo hilo. Hakuruhusu udhanie hivyo kirahisi. Kristo asema, Hapana, mimi sisemi, mimi ni mwalimu, msiniite mwalimu. Mimi sisemi mimi ni nabii… Ninasema mimi ni Mungu katika ubinadamu. “Na watu wanasema, hapana, hapana, ni nabii tu, nabii tunayeweza kumkubali.”[8]

 

Kabla hatujachunguza madai ya Yesu, ni muhimu kuelewa kwamba aliyafanya katika mazingira ya imani ya kiyahudi katika Mungu mmoja. Hakuna myahudi mwaminifu angeamini Mungu zaidi ya mmoja. Na Yesu aliamini Mungu mmoja, akisali kwa Baba yake “Mungu wa Kweli wa Pekee.”[9]

 

Lakini katika maombi hayo, Yesu alizungumzia ya kuwa siku zote na Baba yake. Na wakati Philipo alipomuuliza Yesu kumuonyesha Baba, Yesu alisema, “Philipo, nimekuwa nawe kwa muda mrefu na bado haunijui? Yeyote aliyeniona mimi, amemuona Baba.”[10] Kwa hiyo swali ni “Yesu alikuwa anadai kuwa Mungu wa Waebrania aliyeumba ulimwengu?

 

Yesu alidai kuwa ni Mungu wa Ibrahimu na Musa?

 

Yesu aliendelea kujiita katika namna ambazo ziliwastaajabisha wasikiliza wake. Kama ambayo Piper alivyonukuu, Yesu alitoa kauli za kujiamini, “Kabla ya Abraham kuweko, MIMI NIPO.[11] “Alimwambia Martha na wengine waliomzunguka, “MIMI NI ufufuo na uzima;[12] yeyote aniaminiye, japo amekufa, ataishi”[13] “MIMI NI njia pekee ya uzima”[14] au, “Mimi ni kweli”[15] Haya na mengine kadhaa ya madai yake yalitanguliwa na maneno matakatifu kwa ajili ya Mungu, “MIMI NI (ego eimi).[16] Yesu alimaanisha nini kwa hizo kauli, nini maana na umuhimu wa neno “MIMI NI”?

 

Kwa mara nyingine, lazima turejee kwenye maudhui. Katika maandiko ya kiebrania, wakati Musa alipomwomba Mungu kwa jina lake katika kichaka kiwakacho, Mungu alijibu “MIMI NI”. Alikuwa akijidhihirisha kwa Musa kwamba yeye ni Mungu moja wa pekee ambaye yuko zaidi ya nyakati na aliyekuwapo sikuzote. Kwa kiasi kikubwa Yesu alikuwa akitumia maneno haya matakatifu kujielezea yeye. Swali ni “Kwanini?”

 

Tangu kipindi cha Musa, hakuna myahudi angejiita mwenyewe au kitu chochote kwa kutumia “MIMI NI”. Kama yalivyokuwa matokeo, Madai ya Yesu ya “MIMI NI” yaliwakasirisha viongozi ya kiyahudi. Wakati mmoja kwa mfano, baadhi ya viongozi walieleza kwa Yesu kwanini walikuwa wanajaribu kumuua. “Kwa sababu, wewe mtu tu umejifanya mwenyewe kuwa Mungu.”[17]

 

Matumizi ya Yesu ya jina la Mungu, yaliwakasirisha kwa kiasi kikubwa viongozi wa dini. Pointi ni kwamba hawa wasomi wa Agano la Kale, walijua hasa nini alikuwa akisema – alikuwa akidai kuwa Mungu, kwa uwazi imedhihirika, si kwa kwa maneno yake tu, lakini pia kwa hatua hasi zao kwa maneno hayo.

 

C. S. Lewis mwanzo alimfikiria Yesu kuwa hadithi. Lakini msomi huyu mwerevu, aliyezijua hadithi vizuri, alihitimisha kwamba Yesu alikuwa mtu kweli. Zaidi ya hapo, wakati Lewis alipokuwa akichunguza uthibitisho wa Yesu, alihakikishiwa kwamba sio tu kwamba Yesu alikuwapo kweli, lakini pia hakuwa kama mtu yeyote aliyeishi. Lewis anaandika,

 

“Kisha kuna kitu cha kushangaza kweli” Lewis anaandika, “Miongoni mwa hawa wayahudi, hapo ghafla anatokea mtu anayeendelea kuzungumza kama vile alikuwa Mungu. Anadai kusamehe dhambi. Anasema siku zote aliwakuwapo. Anasema atakuja  kuhukumu ulimwengu katika siku za mwisho.”

 

Kwa Lewis, madai ya Yesu yalikuwa makubwa na mazito sana kufanywa na mwalimu wa kawaida au mwalimu wa dini. (Kwa kuangalia kwa undani zaidi madai ya Yesu kuwa Mungu, angalia “Je Yesu alidai kuwa Mungu?” 

 

Yesu ni Mungu wetu ?

 

Wengine wamebisha kwamba Yesu alikuwa tu akidai kuwa sehemu ya Mungu. Lakini nia ni kwamba sisi sote tu sehemu ya Mungu, na ndani yetu kuna mbegu ya utakatifu, hiyo si kwa urahisi kuwa ni maana inayowezekana kwa yale maneno na matendo ya Yesu. Mawazo hayo ni kudhania kimarejeo, na ni mageni/tofauti na mafundisho yake, tofauti na imani zake, na tofauti na uelewa wa wafuasi wake wa mafundisho yake.

 

Yesu alifundisha kwamba yeye ni Mungu katika namna ambazo wayahudi walimwelewa Mungu na namna ambayo maandiko ya waebrania yalivyomwelezea Mungu, sio kwa jinsi ambayo harakati za kizazi kipya kinavyomwelewa Mungu. Si Yesu wala wamsikilizao waliokatishwa kuona nyota, na wakati wanapomzunguzia, walikuwa hawazungumzii nguvu za anga. Kwa ufupi ni vibaya kuelezea upya kitu gani Yesu alimaanisha kuhusu Mungu.

 

Lewis anaeleza,

 

Sasa tuwe wawazi. Miongoni mwa waaminio utukufu wa Mungu wa ulimwengu, kama wahindi, yeyote aweza asema alikuwa sehemu ya Mungu, au aliyekuwa na Mungu, kwa sababu alikuwa myahudi, hakukumaanisha aina ya Mungu, kwa lugha yao, ilimaanisha Mungu kuwapo nje ya ulimwengu aliouumba na bila shaka alikuwa tofauti na kitu kingine chochote. Na unapoelewa hilo, utaona nini huyu mtu alichosema, rahisi kabisa, kitu cha kushangaza ambacho kimekuwa kikinenwa na midomo ya wanadamu.[19]

 

Bila shaka kuna hao ambao wanamkubali Yesu kama mwalimu mkuu, lakini hawataki kumwita Mungu.  Kama mwamini Mungu, tumeona kwamba Thomas Jefferson alikuwa hana tatizo kukubali mafundisho ya Yesu ya maadili huku akikataa Uungu wake.[20] Lakini kama tulivyosema na tutavyochunguza zaidi, ikiwa Yesu hakuwa namna alivyodai kuwa, lazima tutafute sababu zingine ambazo hazikumfanya kuwa mwalimu mkuu wa maadili. Lewis alidai “Ninajaribu hapa kumzuia yeyote asije akasema kitu cha kipuuzi ambacho watu wengi wanasema kumhusu Yeye [Yesu]: “Mimi niko tayari kumkubali Yesu ni Mwalimu Mkuu wa Maadili, lakini sikubali dai lake la kuwa Mungu. ‘Hicho ni kitu kimojawapo tusichotakiwa kusema.”[21]

 

Katika kutafuta kwake ukweli, Lewis alijua kwamba hawezi kuwa na namna zote mbili za ukuu wa Yesu. Aidha Yesu alikuwa yule – Mungu aliyedai kuwa, katika mwili au madai yake hayakuwa kweli! Na kama hayakuwa kweli, Yesu asingeweza kuwa Mwalimu Mkuu wa Maadili. Angekuwa aidha anadanganya kimataifa? Au angekuwa mwendawazimu akidai namna mbalimbali za Uungu.

 

Yesu hakudanganya

 

Hata wakosoaji wakuu wa Yesu wamemwita mwongo. Kashifa hiyo kwa hakika haimfai Yesu mwenye maadili makuu na mafundisho ya hadhi ya juu. Lakini ikiwa Yesu si yule anayedai kuwa, lazima tuthibitishe uwezekano kwamba alikuwa akidanganya kila mtu kimataifa!

 

Mojawapo ya kazi za kisiasa zenye ushawishi mkuu za nyakati zote ziliandikwa na Niccolo Machiavelli in 1532. Katika msingi wake, Mwanamfalme Machiavelli anaaamini kwamba mamlaka, mafanikio, umaarufu na ufanisi, viko juu ya uaminifu, itikadi na uadilifu.

 

Ingewezekana Yesu Kristo angejenga kanisa lake katika uongo ili kupata mamlaka, umaarufu au mafanikio? Kwa kweli, wapinzani wa Yesu wa kiyahudi, walikuwa wakiendelea moja kwa moja kumfanya Yesu aonekane kama mwongo na tapeli!

 

Swali tunalotakiwa kushughulika nalo ni: Kitu gani kingeweza kumsukuma Yesu kuishi maisha yake yote kuwa mwongo? Alifundisha kwamba Mungu alipingana na kudanganya na unafiki, kwa hiyo asingekuwa akifanya hivyo kumfurahisha Baba yake. Kwa hakika hakudanganya kwa manufaa ya wafuasi wake, kwa sababu wote kasoro mmojawao walikuwa tayari kujitoa mhanga kuliko kukana ukuu wake. (Angalia “Je, Mitume waliamini Yesu ni Mungu? na kwa hiyo tunabakiwa na maelezo ya msingi ya namna mbili, na kila namna ni ngumu.

 

Faida kuu

 

Watu wengi wamedanganya kwa faida binafsi. Kwa kweli, msukumo wa danganyifu nyingi ni kuwa baadhi waliona faida kwao binafsi. Kitu gani Yesu angekuwa ametumainia kwa kudanganya kuhusu utambulisho wake? Mamlaka ndiyo yangekuwa jibu la wazi dhahiri. Ikiwa watu waliamini alikuwa Mungu, angekuwa na mamlaka makubwa. (Hiyo ndiyo sababu viongozi wengi wa kale, kama vile akina Kaizari, walijidai kuwa na asili ya uungu.)

 

Ugumu wa maelezo haya ni kwamba Yesu alikataa majaribu yote ya kuelekea kwenye mamlaka za ulimwengu, badala yake aliwaadhibu hao ambao walitumia vibaya mamlaka na walioishi maisha yao wakiyatafuta mamlaka. Pia aliaamua kwenda kuwafikia watengwa (makahaba na wakoma), wale wasio na mamlaka, akitengeneza jumuiya ya watu ambao umuhimu wao uliokuwa chini ya sifuri. Katika namna ambayo ingeelezwa kuwa kama kituko, yote aliyofanya Yesu na aliyosema yalikwenda upande mwingine mbali na kujitwalia madaraka.

 

Ingeonekana kwamba iwapo mamlaka yangekuwa ndiyo kichocheo kikubwa, angeepuka msalaba kwa gharama zozote. Lakini kwa nyakati kadhaa, aliwaambia wafuasi wake kwamba, msalaba ulikuwa ndiyo safari yake na mpango wake. Je, kufa kwenye msalaba wa Kirumi kungemleteaje mtu mamlaka?

 

Kifo, bila shaka, kinaweka mambo yote katika mwelekeo mzuri. Na wakati wafia dini wamekufa kwa sababu walizoamini, wachache wamekuwa tayari kufa kwa uongo wa waziwazi. Hakika, matumaini yake binafsi ya Yesu yangekuwa yameishia msalabani. Lakini hata wakati wa pumzi yake ya mwisho, hakuacha dai lake la kuwa Mtoto pekee wa Mungu. Msomi wa Agano jipya, J. I. Packer, aweka wazi kwamba habari hii yatangaza uungu wake Yesu.[22]

 

 Mapokeo

 

Hivyo, ingekuwa Yesu alipokuwa juu alidanganya kwa faida binafsi, basi labda dai lake la msingi lingewekwa kuwa msingi wa uongo ili kuacha urithi. Lakini hali ya kupigwa sana kuwa nyakanyaka na kupigiliwa misumari msalabani kungemdhoofishia na kukatisha tamaa/hamu ya kutaka kuwa mtu maarufu kuliko wote duniani.

 

Hapa kuna ukweli mwingine wa kukumbuka usiosahaulika. Ingekuwa kwamba Yesu angeghairi/angeacha madai ya kuwa Mtoto wa Mungu, asingelilaumiwa. Ilikuwa ni dai lake la kuwa Mungu na kukataa kwa kuliacha dai hilo ndilo lililomfanya asulubiwe.

 

Kama ingekuwa ni kuimarisha mamlaka yake na sifa ya kihistoria ndivyo vitu vilivyomsukuma Yesu kudanganya, basi lazime muelezee ni namna gani mtoto wa fundi seramala kutoka katika kijiji maskini cha Yuda angeweza kutarajia matukio ambayo yangelipeleka jina lake kuwa maarufu wa duniani kote. Angejuaje ujumbe wake ungeishi na ungedumu? Wafuasi wa Yesu walikimbia na Petro alimkana. Siyo utaratibu hasa wa kawaida kuacha mapokeo ya kidini.

 

Je, wanahistoria wanaamini Yesu alidanganya? Wasomi wamechunguza maneno na maisha ya Yesu kuona kama kuna ushahidi wowote wa kasoro za maadili katika tabia yake. Kwa kweli hata wakosoaji wakali wanashangazwa na ujasiri wa Yesu na usafi wa maadili.

 

Kulingana na mwanahistoria Philip Schaff, hakuna ushahidi, aidha katika historia ya kanisa au historia ya kawaida kwamba Yesu alidanganya kuhusu chochote. Schaff anadai, “Ni jinsi gani katika namna ya busara makini na uzoefu ingeweza kumfanya mtu mwenye hila, mbinafsi, asiye mwadilifu abuni na aendeleze tabia njema inayoheshimika katika historia, kuanzia mwanzo hadi mwisho ikiwa na sifa kamilifu za ukweli na uhalisia?”[23]

 

Kuendelea na nia ya kumwita [Yesu] mwongo inaonekana ni kama kuogelea kuelekea maporomoko ya juu, na ni kinyume na kila kitu Yesu alichofundisha, alichoishi na alichofia. Kwa wanafunzi wengi, haina maana hata kidogo [kusema Yesu ni mwongo]. Pia kukana madai ya Yesu, mtu lazima aje na maelezo ya kutosha. Na ikiwa madai ya Yesu si ya kweli, na kwamba Yesu alikuwa hadanganyi, basi hatua iliyobaki ni kusema kwamba alikuwa anajidanganya mwenyewe.

 

Yesu angeweza kuwa anajidanganya ?

 

Albert Schweitzer, ambaye alitunukiwa Nishani ya Nobeli mwaka 1952 kwa juhudi zake za kibinadamu, alikuwa na maoni yake binafsi kuhusu Yesu. Schweitzer alidai kwamba uendawazimu uliambatana na madai ya Yesu, kudai kuwa Mungu! Kwa maneno mengine, Yesu hakuwa sahihi kuhusu madai yake lakini hakudanganya kimataifa. Kulingana na nadharia hii ya kubuni, anadai Yesu alijidanganya hadi kufikia hatua ya kuamini alikuwa Masiha!

 

Lewis anafikiria wazo hili kwa makini sana. Anachambua kwamba ikiwa madai ya Yesu hayakuwa kweli, basi lazima alikuwa mwendawazimu. Lewis anatoa sababu kwamba kama mtu aliyedai kuwa Mungu asingekuwa mwalimu mkuu wa maadili, angekuwa aidha mwendawazimu sawa na mtu anayesema yeye ni yai, au vinginevyo angekuwa ni shetani wa Jehanam.[24]

 

Wengi wamesoma maisha na maneno ya Yesu na wamemkiri kwamba ni mtu tu mwenye busara sana. Ingawaje maisha yake mwenyewe yalishutumiwa na upotofu na ukosoaji binafsi, mwanafalsafa maarufu wa kiFaransa Jean Jacques Rousseau (1712 – 78) amekiri tabia kuu takatifu ya Yesu na yenye akili timamu akisema “Wakati Plato alipoelezea kuwa Yesu ni mwenye haki, alielezea tabia halisi ya Yesu. Ikiwa maisha na kifo cha Socrates ni yale ya huyo mwanafalsafa, basi maisha na kifo cha Yesu ni yale ya Mungu.”[25]

 

Bono anahitimisha kwamba ‘mwendawazimu” ndio kitu cha mwisho ambacho mtu angemdhania Yesu kuwa.

 

“Hivyo kitu unachobakia nacho ni aidha kusema Kristo alikuwa ndivyo alivyosema, alikuwa ndiye, au mwendawazimu. Ninamaanisha, tunasema mwendawazimu katika dhana ya Charles Manson…. Sitanii hapa. Wazo kwamba maendeleo yote ya ustaarabu kwa zaidi ya nusu ya dunia yangeweza kubadilika ama kubadilishwa na mwendawazimu! Kwangu mimi huo ni uongo uliozidishwa kipimo.”[26]

 

Eti kwamba Yesu alikuwa mwongo au mwendawazimu, kwamba alikuwa ni Mtoto wa Mungu? Jefferson angekuwa sahihi kumwita” Yesu mwalimu wa maadili pekee” huku akina uungu wa Yesu? Kitu cha kufurahisha, watu waliomsikia Yesu wote, wafuasi na maadui zake hawakuwahi kumfikiria Yesu kuwa ni mwalimu tu maadili. Yesu amepata mambo matatu kwa watu waliokutana nao: chuki, vitisho au kuabudiwa.

 

Madai ya Yesu yametulazimisha kuchagua. Kama ambavyo Lewis alivyonena, hatuwezi kumweka Yesu katika kundi la kuwa tu ni kiongozi mkuu wa dini or mwalimu wa maadili. Ukosoaji huu wa kizamani unatupa changamoto kusafisha akili zetu kuhusu Yesu,

 

“Lazima ufanye uamuzi wako sasa. Aidha huyu mtu alikuwa, au ni mwana wa Mungu: au vinginevyo ni mwendawazimu au ni kitu kingine. Unaweza kumnyamazisha Yesu kwa kumfanya mpumbavu, unaweza kumtemea mate, kumuua kama pepo au unaweza kuanguka miguuni pake Yesu na kumwita Bwana na Mungu. Lakini tusilete upuuzi wowote wa kumdhalilisha Yesu kuwa ni mwalimu tu mkuu mwanadamu. Hajaacha hivyo wazi kwetu. Hakukusudia hivyo.”[27]

 

Katika ukristu pekee, Lewis amechunguza wazo linalotafakari utambulisho wa Yesu, akihitimisha kwamba Yesu kwa hakika yuko vile vile alivyodai kuwa. Uchunguzi wake makini wa maisha na maneno ya Yesu ulipelekea huyu mtu mwerevu  akane imani yake ya zamani ya kutoamini na akaongoka kuwa mKristu wa kweli dhati anayeamini.

 

Swali kuu katika historia ya mwanadamu ni, “ni nani ni Yesu Kristo wa kweli?” Bono, Lewis na wengine wengi wasiohesabika wamehitimisha kwamba Mungu alitembelea sayari katika umbo la mwanadamu. Lakini kama hivyo ni kweli, basi tungemtarajia kuwa hai leo. Na hivyo ndivyo ilivyo kwa hakika na jinsi wafuasi wake wanavyoaamini.

 

 Yesu alifufuka toka katika Wafu?

 

Mashahidi wa macho kwa Yesu Kristo kwa kweli walizungumza na walitenda kama walivyoamini, alifufuka toka katika wafu baada ya kusulubiwa kwake. Ikiwa walikosea basi uKristu umeanzishwa kwa uongo? Lakini kama walikuwa sahihi, muujiza huo ungethibitisha yote Yesu aliyosema kuhusu Mungu, kuhusu yeye na kutuhusu sisi.

 

Lakini ni lazima tuamini ufufuko wa Yesu Kristo kwa imani pekee, au kuna ushahidi wowote wa kihistoria? Wakosoaji kadhaa walianza uchunguzi kwenye kumbukumbu za kihistoria kujaribu kuona kama kweli maelezo ya ufufuko yalikuwa uongo.

 

Itaendelea

 

 

No comments: