JINSI YA KUFAHAMU MIUJIZA YA SHETANI
Nyakati tulizonazo leo,zinzitwa NYAKATI ZA HATARI..Biblia
inasema kwamba siku hizi za mwisho,wengine watajitenga na imani,wakisikiliza
ROHO ZIDANGANYAZO na MAFUNDISHO YA MASHETANI (2TIMOTHEO 3:1,1TIMOTHEO 4:1).Roho
zidanganyazo zitafanya kila namna,kutudanganya,ili kile cha Mungu tukiite cha
shetani,na kile kilicho cha shetani,tukiite cha Mungu.Leo,tunazungukwa na watu
wanaosema,jihadhari usiende kule.Ingawa kuna miujiza mingi huko,miujiza
hiyo,inatokana na ROHO CHAFU au MASHETANI.Mtu yule,anatoa pepo kwa kutumia DAWA
au HIRIZI.Kutokana na mambo yake ya ushirikina,mtu akienda kumsikiliza mara
moja tu,yeye naye ananyweshwa roho chafu na kudanganyika.Maneno haya,yanaweza
yakawa ya kweli au yasiwe ya ukweli.Pasipokuwa na mafundisho,hatuwezi
kupambanua kilicho cha Mungu na kilicho cha Shetani.Pasipo kuoambanua,tunaweza
tukamwita mtu wa Mungu kuwa ni PEPO na kwamba anatoa pepo kwa BEELZEBULI,mkuu
wa pepo,kwasababu tu HAFUATANI NASI (YOHANA 8:48-49; MATHAYO 12:22-24;LUKA
9:49-50).Mambo haya,hayapaswi kuwa hivi.Kwa sababu hii basi ni makusudi ya
Mungu ujifunze somo hili.Tunaligawa somo hili katika vipengele vitatu;-
UWEZEKANO WA SHETANI KUFANYA MIUJIZA.
JINSI YA KUIFAHAMU MIUJIZA YA MUNGU.
HUKUMU YA WATUMISHI WA SHETANI
1.UWEZEKANO WA SHETANI KUFANYA MIUJIZA.
Shetani, ana uwezo wa kufanya ishara na miujiza kadhaa,kwa
kipimo kidogo cha uwezo ulio na mpaka.Roho chafu,roho za mashetani,zina uwezo
wa kufanya ishara (UFUNUO 16:13-14).Wakati wa dhiki kubwa,roho za
mashetani,zitafanya ishara kubwa,hata kufanya moto kutoka mbinguni uje juu ya
nchi mbele ya wanadamu (UFUNUO 13:11-13).Wakati wa wana wa Israeli, walipokuwa
hawajatoka Misri,waganga na wachawi wa Farao,walifanya miujiza kwa uwezo wa
Shetani:-
(a). Wachawi
hao,walipozibwaga fimbo zao chini,ziligeuka kuwa nyoka kwa mfano wa muujiza
alioufanya Mungu kwa kuwatumia Musa na Haruni (KUTOKA 7:8-12).
(b) Wachawi
hawa,walifanya muujiza wa kubadili maji kuwa damu,kwa mfano wa muujiza
alioufanya Mungu kwa kuwatumia Musa na Haruni (KUTOKA 7:19-22)
Hata hivyo,pamoja na wachawi na waganga hawa kufanya miujiza hii,walikuwa na mpaka
katika uwezo wao.Wachawi hawa,walishindwa kufanya mavumbi ya nchi kuwa chawa
kwa mfano wa Musa na Haruni,na vulevile walishindwa kuzuia majipu
yaliyosababishwa na muujiza wa Mungu kupitia kwa Musa,kuwapata na wao
pia.Wakakiri kwamba uwezo wa Mungu uko juu mno kuliko uwezo wao (KUTOKA
8:16-19;9:8-11).Shetani hana uwezo wote,hawezi kutenda mambo yote.Mungu wetu
ana uwezo mkuu mno.Fimbo ya Haruni,ilizimeza fimbo za wachawi,kudhihirisha
uwezo wa Mungu ulivyo mkubwa mno kuliko majeshi yote ya Shetani (KUTOKA
7:11-12).Ni muhimu kufahamu kwamba miujiza ya Shetani,inalengo la
KUWAPOTEZA,kama yamkini hata walio wateule.Ni nguvu ya upotevu,ya kuwafanya
wale wote wasioipenda kweli ya Neno la Mungu KUPOTEA (MATHAYO
24:24;2WATHESALONIKE 2:7-12).Ili basi tusipotezwe na roho hizi za mashetani,ni muhimu
kuifahamu Kweli,ili tuweze kupambanua miujiza ya mashetani na miujiza ya
Mungu.Hili sasa linatuleta katika kipengele cha pili cha somo letu.
2. . JINSI YA KUIFAHAMU MIUJIZA YA MUNGU.
Ili kuifahamu na kuipambanua miujiza ya mashetani.itakuwa
vema kujifunza alama zitakazotuwezesha kuifahamu miujiza ya Mungu.Tukiweza
kufahamu namna ya kupambanua miujiza ya Mungu,itakuwa ni rahisi kufahamu
kinyume chake,na kuifahamu miujiza ya mashetani.ZIKO ALAMA KUMI (10) za
kutuwezesha kuifahamu miujiza ya Mungu.Alama zote hizi,lazima zionekane katika
huduma yoyote inayotumiwa na Mungu kufanya miujiza.Tukiziona alama zote hizi
kumi katika huduma yoyote ya miujiza,tujue huduma hiyo niya Mungu,na hatupaswi
kusema mtu huyo wa Mungu anatumia roho chafu au anatoa pepo kwa Beelzebuli,mkuu
wa pepo.Alama hizi kumi ni hizi zifuatazo:-
1. .Mtu
anayetumiwa kufanya miujiza ya Mungu, lazima mwenyewe awe ameamini na
kuokolewa; akikiri mwenyewe wokovu ulio katika Kristo Yesu, na kuushuhudia
ishara au miujiza ya Mungu, hufuatana nao WAAMINIO tu, au waliookolewa (MARKO
16:17).Mtu yeyote ambaye hajaokoka, hawezi kufanya miujiza inayotokana na
Mungu.Miujiza anayoifanya mtu yeyote ambaye hajaokoka, ni miujiza ya shetani.
2. .Huma yoyote ya
miujiza ya Mungu, lazima iambatane na Biblia au Neno la Mungu, kwa kuwa Neno
la Mungu ndiyo dawa ya ugonjwa na tena
ndilo linalofanya miujiza(ZABURI 107:20; MITHALI 4:20-22; YOHANA 6:63). Mtu anayetumiwa kufanya miujiza ya
Mungu, ataiamini Biblia na kuifanya kuwa msingi wa utendaji wake wote. Huduma
yoyote ya miujiza isiyoambatana Biblia, inatokana na Shetani.
3. Huduma yoyote
ya miujiza inayotokana na Mungu, LAZIMA iambatane na KUHUBIRI NA KUFUNDISHA
Neno la Mungu. Mtu yeyote anayedai kwamba yeye hakupewa kuhubiri Neno, ila
amepewa karama ya kutenda miujiza tu, huyo anatumiwa na Shetani (LUKA 4:18; 5:17; 9; 8:1-2; MATHAYO 10:7-8). Huduma yoyote ya miujiza ya Mungu,
lazima iambatane kuhubiri kwamba watu watubu dhambi zao na kuziacha, na
kuokolewa. Kinyume cha hapo, ni huduma ya Shetani (MARKO 4:6;12-13).
4. Miujiza yoyote
ya Mungu, LAZIMA ifanyike kwa jina la YESU (LUKA 10:17; MATENDO 4:30; MARKO
16:17; MATENDO 3:6; 4:10; 3;13,
16, 16:18).
5. Miujiza yoyote
ya Mungu, hutumika kuwaleta watu kwa Bwana Yesu na kuwafanya wawe wanafunzi wa
Yesu, na kuwafundisha kudumu katika kanisa linalohubiri wokovu (MATENDO 5:12,
14; 2:41-43; 6:7-8; 8:5-8, 12). Miujiza
isiyo na lengo hili ni miujiza ya Shetani.
6. Mtu yeyote
anayetumiwa kufanya miujiza ya Mungu, lazima afanye huduma yake kwa
kushirikiana na makanisa yanayohubiri wokovu, ili apate kutoa ripoti ya huduma
yake inavyokwenda na kuwajibika (MATENDO 14:27; 21:17-19; 1WAKORINTHO 14:29).
7. Miujiza ya
Mungu, hutusogeza katika kumtumikia Yesu Kristo na kushika maagizo yake, na
kutufanya kuwa watakatifu kama yeye alivyo mtakatifu. Miujiza yoyote
inayoambatana na maagizo yoyote yaliyo kinyume na Neno la Mungu, kama kutumia
sanamu za watakatifu, kufukiza uvumba, kutumia rozari au maji ya Baraka, kuzuru
makaburi, kuwaomba wafu tuwaombee n.k; haitokani na Mungu (KUMBUKUMBU
13:1-4).Mafundisho ya mtu anayetumiwa kufanya miujiza ya Mungu, hutufundisha
kuwa watakatifu, na kuwa mbali na mapenzi ya Mataifa. Wote waliotumiwa sana na
Mungu kufanya miujiza kama Paulo, Petro, Yakobo na Yohana, walifundisha hivyo
(WARUMI 12:1-2; 1YOHANA 2:15-17; 1 PETRO 1:14-16; 2:12; 4:2-3; YAKOBO 4:4; 1
WAKORINTHO 4:3-4).
8. Miujiza ya
Mungu hutolewa bure, hainunuliwi (MATHAYO 10:8; 2 WAFALME 5:14-16; DANIELI
5:16-17; 1 WAFALME 13:6-8; MATENDO 8:18-20). Namna yoyote ya kuomba hela ili
kununua muujiza ni kinyume na mpango wa Mungu .Hata kama tutaona wakiuza
vitambaa,leso na sabuni zilizoombewa ili zitusaidie, hatuna budi kujua mapanzi
ya Mungu kwa watumishi wake ni kutoa huduma ya maombezi bure. Huduma yoyote
inayochangisha mchango au kiingilio kwa ajili ya semina ya Neno la Mungu hiyo
siyo huduma ya kimungu, ni huduma ya Shetani. Mungu anataka injili iwafikie
watu wote.Mfano 1 wa huduma ya shetani ni huduma ya babu wa Loliondo. Bila
kutoa sh: 500 usingeweza kupata msaada.Pia miujiza ya Mungu inatokana
na Neno la Mungu kama tulivyoona hapo juu. Miujiza ya Mungu inakuwa na lengo la
kuwaleta watu kwa Yesu.Watu wanaokuja kutafuta msaada kwa Yesu sharti waongozwe
kutubu dhambi zao
kwanza ili kuwapatanisha na Mungu kwa ajili ya kufungua
mlangio wa Miujiza yao.
9. Miujiza ya
Mungu humtukuza mwana wa , Yesu kristo (YOHANA 11:4), wale wanaotumiwa na Mungu
kufanya miujiza ya Mungu hubaki wanadamu na wao kukiri hivyo, na kumpa Mungu
utukufu(MATENDO 14:8-18). Tunapomuona
mtu akichukua utukufu kana kwa mba yeye ndiye anayetenda miujiza ndipo
tunatambua kuwa huyo si mtumishi wa Mungu.
10. Maisha ya mtu
anyetumiwa na Mungu kufanya miujiza yanapaswa kuwa sawasawa na Neno la Mungu.
Watu wanaotumiwa na Shetani kufanya miujiza, huambatana na dhambi NNE
zinazoonekana upesi-uzinzi au uasherati (1 WAKORINTHO 6:15-17), maneno ya
kihuni (YAKOBO 3:10-12), maisha yaliyo sawa na mataifa katika kuvaa na kutenda
(WARUMI 12:2; 1 PETRO 2:12; YAKOBO 4:4),
maisha yasiyo na uaminifu katika masuala ya fedha na kusema uongo (NEHEMIA 7:2)
3. HUKUMU YA
WATUMISHI WA SHETANI
No comments:
Post a Comment