CHAKULA CHA WATOTO
Tunaendelea kujifunza Biblia katika sura ya 15 ya kitabu cha MATHAYO.
Ingawa kichwa cha somo letu ni “CHAKULA CHA WATOTO“, hata hivyo tuna mengi
zaidi ya kujifunza. Tutaliangalia somo letu la leo katika vipengele vitatu:-
(1) ALAMA ZA MAFARISAYO;
(2) MPANGO WA MUNGU WA WOKOVU;
(3) CHAKULA CHA WATOTO.
(1) ALAMA ZA MAFARISAYO
Katika sura ya 15 pekee ya kitabu hiki cha Mathayo,
“Mafarisayo” wanatajwa katika MST. 1 & 12. Katika sura zilizotangulia pia
tumeona Yesu akitaja sana habari za “Mafarisayo”. Katika MATHAYO 16:11-12, Yesu
anatuonya kujilinda na mafundisho ya Mafarisayo. Sasa basi, tutawezaje
kuwafahamu Mafarisayo na mafundisho yao? Tutawafahamu kwa alama zifuatazo:-
1. HULITANGUA NENO LA MUNGU NA KUYASHIKA MAFUNDISHO YALIYO
MAAGIZO YA WANADAMU (MATHAYO 15:6-9; MARKO 7:13; YOHANA 17:17);
2. HUMHESHIMU MUNGU KWA MIDOMO TU ILA MIOYO YAO IKO MBALI
NAYE (MATHAYO 15:8-9; TITO 1:16; YOHANA 4:23-25);
3. KAZI YAO NI KUTAFUTA MAKOSA (MATHAYO 15:2; 12:1-2; LUKA
14:1-3; MITHALI 28:9);
4. HUJIFANYA WANAFUATA MAAGIZO YA MUSA HUKU WAKIMKANA (MARKO
7:10-12; TITO 3:4-8; 1 WAKORINTHO 10:14) – Musa aliandika habari za Yesu
(YOHANA 1:45; 5:46). Musa alisema kwamba watu wamsikie Yesu atakapokuja kwao na
kwamba mtu yeyote ambaye hatasikia neno la Yesu, Mungu atalitaka kwake
(KUMBUKUMBU LA TORATI 18:15, 18-19; linganisha na YOHANA 12:48; MATHAYO 17:1-5);
5. HUTAWADHA KWA NJE TU NA KUACHA MIOYO YAO MICHAFU (MARKO
7:4; MATHAYO 23:25-28).
(2) MPANGO WA MUNGU WA WOKOVU (MATHAYO 15:21-24)
“Sikutumwa ila kwa kondoo waliopotea wa nyumba ya Israeli”,
haimaanishi kwamba Yesu hakuja kwa ajili ya wengine wasio Waisraeli. Katika
mpango wowote unaopangwa, yeye anayeupanga ana haki kuamua kwamba ataanzia wapi
katika kuutekeleza na anaweza kuweka awamu mbalimbali za utekelezaji wa mpango
huo. Katika Mpango wa Mungu wa wokovu, awamu ya kwanza ya utekelezaji wa mpango
huo ilikuwa kuleta wokovu (unaojumuisha uponyaji) kwanza kwa Waisraeli (YOHANA
1:11; MATHAYO 10:6). Awamu ya pili ilikuwa kuwapa ulimwengu wote uliosalia
wokovu (MATHAYO 21:423; YOHANA 10:16; 11:49-52; WARUMI 1:16; 9:24-30; MATENDO
15:13-18; WAEFESO 3:1-11).
(3) CHAKULA CHA WATOTO (MATHAYO 15:21-28)
Watu wasio Waisraeli yaani Mataifa, walipewa jina “MBWA” na
Waisraeli. Yesu Kristo alilitumia jina hili kwa sababu ulikuwa usemi wa kawaida
ulioeleweka na kutumiwa na kila mtu Nyakati za Biblia (1 SAMWELI 17:43; 2
SAMWELI 3:8, 9:8). Jina “MBWA” halikuwa tusi ila lilieleza hali halisi
iliyokuwapo. Mbwa hawakuwa wakitunzwa kwa kutengenezewa chakula kizuri na wale
waliowafuga ila walitupiwa makombo tu. Hawakuruhusiwa kama ilivyo leo kukaa
ndani ya nyumba kuwa karibu sana na wanadamu. Mataifa waliitwa “mbwa” kwa jinsi
ambavyo hawakuwa na “haki ya ndani” walizokuwa nazo Waisraeli. Mungu
alihesabiwa kukaa katika nyumba ya Waisraeli peke yao. Hao tu ndio waliokuwa
watoto wake (1 WAFALME 8:13). Baba anawajibika kuwapa kwanza watoto wake
chakula. Ingawa anaweza kumpa chakula mtoto wa wengine hata hivyo kizuri
kitakuwa cha watoto wake kwanza.
Watu tuliookoka ni watoto wa Mungu (YOHANA 1:12). Kutokana
na kuwa watoto, chakula cha uponyaji, kufunguliwa kutokana na nguvu za giza
n.k.; vyote hivi ni HAKI YA WATOTO KATIKA FAMILIA YA MUNGU. Kama hapa mbwa
alipewa makombo basi sisi watoto tutapewa uzima tena uzima tele. (MATHAYO
7:7-11; MARKO 9:23; ZABURI 103:13; ISAYA 49:14-16).
barikiwa. Kwasababu hii share ujumbe huu kwa kubonyeza neno“
share” lililopo chini ya “note” hii, kwa kufanya hivyo ujumbe huu utafika kwa
watu wengi. Hakika, Baraka za Mungu zitakuwa nawe.. ( FULL GOSPEL)
No comments:
Post a Comment