JEHANUM YA MOTO
Yesu Kristo anatufundisha waziwazi kuhusu Jehanum ya moto,
akituonya kumwogopa Mungu mwenye uwezo wa kututupa Jehanum. Anaendelea kutuonya
kwamba, ni heri kukubali lolote lile litupate kuliko kwenda kwenye mateso
makali ya Jehanum (LUKA 12:5, MATHAYO 5:22, 29-30). Maandiko pia yanaendelea
kusisitiza kwa msisitizo mkubwa kwamba, ni jambo la kutisha kuanguka katika
mikono ya Mungu aliye hai na kutupwa katika Jehanum ya moto (WAEBRANIA
10:26-27, 31). Jehanum hii ya moto inaitwa pia kuzimu (ZABURI 9:17) na tena
inaitwa Tofeni (ISAYA 30:33). Hatupaswi kulipuuza jambo hili na kulifanya juu
juu tu. Kwa sababu hii, leo, tutajifunza kwa undani kuhusu Jehanum ya moto, na
tutaligawa somo letu katika vipengele vinne:-
(1) HUKUMU BAADA TU
YA KUFA
(2) JEHANUM YA MOTO
IKO WAP?
(3) HALI HALISI YA
JEHANUM NA WALE WALIOKO HUKO
(4) JINSI YA
KUIKWEPA JEHANUM YA MOTO
( 1 ). HUKUMU BAADA YA KUFA
Biblia inaeleza waziwazi kwamba mtu anapokufa, sekunde
ileile ya kufa kwake anakabiliwa na hukumu (WAEBRANIA 9:27). Watu wanaofundisha
kinyume na kweli ya neno, hufundisha kwamba mtu anapokufa analala tu na hakuna
lolote la hukumu ya mara moja. Wanatumia maandiko yanayozungumzia kulala kwa
kuyatafsiri isivyo (MATHAYO 27:52; 1 WAKORINTHO 15:20; YOHANA 11:11-14 n.k ) na
pia wanasema wafu hawajui lolote kwa kutumia maandiko kama MHUBIRI 9:5. Ilivyo
ni kwamba kinachobaki kaburini ni mwili tu. Nafsi na roho ya mtu huondoka kwa kuvalishwa mwili mwingine (
1WAKORINTHO 15:40 ). Mwili unaobaki kaburini ndiyo ambao umelala haujui lolote
na hauna kumbukumbu, lakini pasipo mwili huo mtu atamwona Mungu ikiwa ameishi
katika mapenzi yake (AYUBU 19:26). Mwili hubaki kaburini, lakini roho ya mtu
huondoka (MHUBIRI 12:7). Ikiwa mtu ameishi katika mapenzi ya Mungu mara tu ya
kufa huchukuliwa mbinguni na malaika kwa kutumia magari maalum ya mbinguni
(LUKA 23:43; 16:22; 2WAFALME 2:11-12;
ZABURI 68:17; WAEBRANIA 1:7, 14). Ikiwa ameishi katika dhambi hukumu yake huwa
kutupwa katika Jehanum ya moto mara tu baada ya kufa (MITHALI 9:13-18; ISAYA
5:11-15; MITHALI 17:24-27).
( 2 ). JEHANUM YA MMOTO IKO WAPI?
Mtu anapokufa tu, huwa kwenye njia panda. Kila mmoja hupenda
kwenda mbinguni, hata hivo ikiwa jina lake haliko katika kitabu cha uzima cha
mbinguni, hulazimika kwenda Jehanum ya moto. Mtu anayetakiwa kwenda motoni
huchachamaa na kukataa kwenda kwenye njia mbaya inayotisha ya motoni na
hulazimika kukamatwa na kutupwa Jehanum (UFUNUO 19:20; 20:10). Mbinguni ni juu
(mbingu ya tatu) lakini kuzimu au Jehanum ya moto ni chini (pande za chini za
nchi) 2WAKORINTHO 12:1-4; ITHALI 15:24; ZABURI 63:9; EZEKIELI 31:14.
( 3 ). HALI HALISI YA JEHANUM NA WALE WALIOKO HUKO
Jehanum ya moto ni kuzimu au shimo kubwa na refu sana
lililojaa moto. Moto huu huwashwa mfululizo kwa pumzi ya Bwana (ISAYA 14:15;
30:33). Moto ni mkali kuliko moto wowote tunaoufahamu duniani, uwe gesi, umeme,
makaa yam awe au lolote jingine (WAEBRANIA 10:27). Moto huu ni mweusi unaosababisha
giza na kufanya mtu awaone wenzake wachache tu wa karibu naye (MATHAYO 11-12;
22:13; 25:30 YUDA 1:6). Moto huu una uwezo wa kula na kutafuna, kwa hiyo
huwatafuna au kuwala wale walioko motoni (KUMBUKUMBU LA TORATI 32:22; WAEBRANIA
10:36-27). Hata hivyo, kama jinsi ambavyo chumvi inavyozuia nyama kuharibika,
moto humtafuna mtu lakini hamaliziki (MARKO 9:43-49). Ni moto wa milele (MATAYO
25:41). Mafundisho potofu ysnswafariji watu na kusema eti mtu ataunguzwa na
moto na kutoweshwa au kupotea na kuangamia
kabisa na ndiyo mwisho wake. Wanatumia maandiko kama MATHAYO 10:28 (
kuangamizwa ) na YOHANA 3:16 ( kupotea ). Kuangamia hakumaanishi kualizika
kabisa (ESTA 4:16). Kondoo akipotea haimaanishi hayupo kabisa ila ametengwa na
mchungaji (angalia ISAYA 57:1-3). Vilevile neno “kuharibu” linapotumika
kuhusiana na adhabu ya milele halina maana ya kufanya kitu kisiwepo, bali ni la
kuzdhibu vikali ( 1WAKORINTHO 3:16-17 ). Waalimu hawa wa uongo hufundisha pia
kwamba ati watu watatoweshwa kama moshi baada kwa kuunguzwa kwa kutumia ZABURI
37:20. Kutoweshwa hapa ni kutenganishwa mbali na Mungu. Moto wa milele,
huambatana na madini yanayoitwa kiberiti (lugha ya kitaalam, “sulphur”). Madini
haya yakiwaka huwa kama mpira na hutoa harufu kama ya mayai yaliyooza. Harufu
ya namna hii inafunika kuzimu yote. Siyo hayo tu, katika moto huu wamo funza
maalum ambao huwatafuna watu na kufanya matundu mengi katika miili yao
wakiingia na kutoka. Hii hufanya sura zao kuwa mbaya mno kama madude tu! (ISAYA
14:11; MARKO 9:43-49; ISAYA 66:24). Jehanum ya moto, huitwa pia mauti ya pili
(UFUNUO 21:8). Uchungu wa mauti unaompata mtu anapokufa, huwa juu ya mtu
motoni, milele na milele (UFUNUO 20:10). Watu walioko motoni hujawa wakati wote
na vilio na tena husaga meno yao kama mtu anayeona baridi kali MATHAYO 8:12).
Kuzimu, urikalo ni pigo lif urikalo ambalo huwachukua wenye dhambi asubuhi,
mchana na usiku (ISAYA 28:15, 18-19). Walioko motoni wanajifahamu, na
kuwakumbuka wenzao waliowaacha duniani na tena hutoa ndimi zao nje wakitamani
maji kidogo kupoza ulimi (LUKA 16:19-24). Juu ya yote hayo, katika vilio vyao,
humwomba Mungu awahurumie na kuwasamehe lakini Yeye amekwishasema, “Nami jicho
langu halitaachilia, wala sitaona huruma” (EZEKIELI9:10;8:18).
USEMI NA FIKRA ZA WALE WALIOKO MOTONI
Watu walioko motoni hutamani mtu mmoja kati yao aje
awashuhudie ndugu zao ili wayoache dhambi na kukwepa mateso yao (LUKA
16:27-31). Wale walioko huko wajiopata mafundisho haya kabla, husema, “Jinsi
nilivyochukia maonyo, na na moyo wangu
ukadharau kukemewa; wala sikuisikia sauti ya waalimu wangu, wala sikuwategea
sikio langu walionifundisha (MITHALI 5:11-13)” Wakimwona yeyote anayejiunga
nao, humwambia, “Jew ewe umekuwa dhaifu kama sisi! Wewe nawe ummekuwa kama
sisi!” ( ISAYA 14:9-10).
WALIO MBINGUNI HUPEWA NAFASI YA KUWACHUNGULIA
Walioko mbinguni watatoka kidogo kuwaangalia (ISAYA 66:24)
ila hawatakuwa na machozi yoyote juu
yao.
TOFAUTI KATI YA JEHANUM YA MOTO NA ZIWA LA MOTO
Jehanum ya moto ni tofauti na ziwa la moto linalotajwa katika
UFUNUO 20:14-15; 21:8 kwa jinsi ileile mbingu ya sasa ilivyo tofauti na mbingu
mpya inayotajwa katika UFUNUO 21:1. Ziwa la moto kwa sasa halina mkazi ndani
yake. Watakaokuwa wa kwanza kuingia humo watakuwa mnyama (Mpinga Kristo) na
nabii wa uongo (UFUNUO 19:20). Kisha atafuata ibilisi ambaye atatupwa humo
baada ya vita ya Gogu na Magogu (UFUNUO 20:7-10). Baada ya hapo kutafuata
hukumu ya jiti cha enzi, kikubwa cheupe. Hukumu hii itatolewa baada ya ufufuo
wa pili au ufufuo wa hukumu ambao utawafufua walioko Jehanum ya moto.Baada ya
hawa kuelezwa kwa nini wamehukumiwa adhabu ya matesoya milele, ndipo
watakapotupwa katika ziwa la moto. Mateso yaliyoko ziwa la moto ni zaidi sana
kuliko mateso ya Jehanum ya moto. Ni kama Jehanum walikuwa mahabusu na sasa wanapelekwa
gerezani. Kama mbingu mpya itakavyokuwa nzuri zaidi kuliko mbingu ya sasa,
vivyo ziwa la moto litakuwa na mateso yaliyokithiri kuliko Jehanum ya moto.
( 4 ). JINSI YA KUIKWEPA JEHANUM YA MOTO
1 .Kuungama dhambi na kuziacha (MITHALI 28:13).
2. Kulishika Neno la Mungu kwa kufanya maagizo yote ya Mungu
na kuwakata wafariji wenye kutaabisha
wanaosema kufanya hili na lile siyo lazima
( YOHANA 8:51; ZABURI 119:6; AYUBU 16:1-2 ).
3. Kutohesabu sheria kuwa kutu kigeni. Kukubali kuongozwa na
sheria ya Kristo. Hakuna mwanafunzi asiyeishi kwa sheria ( HOSEA 8:12; WAGALATIA 6:2; ISAYA 8:16 ).
4. Kuwa mtakatifu na kutoifuatisha namna ya dunia hii katika
mavazi, usemi, matendo n.k. ( WAEBRANIA 12:14;
WARUMI 12:2; YAKOBO 4:4; 1YOHANA 2:15-17 )
JE! WEWE NAWE UMEKUWA DHAIFU KAMA SISI!
ISAYA 14:9-10
No comments:
Post a Comment